- 9,938 viewsDuration: 3:50Kijana mmoja ambaye alifahamika kama jambazi sugu aliyekuwa akiendeleza wizi wa mabavu katika mitaa ya ziwa la ngome na maweni huko nyali kaunti ya mombasa, amegeuza mkondo wa maisha baada ya kunusurika kifo. Dennis Munyoki, mwenye umri wa miaka 20, alikodolea macho kifo alipopigwa na umati baada ya kufumaniwa akiiba. Tukio hilo limimfanya ajirudi na akaamua kuacha uhalifu na kurudi shuleni. Dennis ni miongoni mwa vijana 13 waliojisalimisha kwa polisi na kuamua kuasi uhalifu.