Jamii ya Maa yapeleka utamaduni zao Kwale kukuza utalii

  • | Citizen TV
    307 views

    Utumaduni wa jamii ya Maa unatambulika kukolea kwenye kaunti za Narok, Kajiado, Samburu na Laikipia ambako watu wa jamii hiyo wanapatikana kwa wingi. Lakini sasa utamaduni huo umepenya hadi kaunti ya Kwale ili kuimarisha utalii katika fuo za Diani. Aidha watu wa jamii hiyo hufanya uchaguzi kwa mfumo wa mlolongo ili kumchagua kiongozi wao eneo hilo