Skip to main content
Skip to main content

Jamii yahimizwa kukomesha unyanyapaa kwa walemavu

  • | Citizen TV
    120 views
    Duration: 1:52
    Waziri wa Jinsia na maswala ya Watoto, Hanna Cheptumo, ametoa wito wa wanajamii kuwalinda watoto walio na ulemavu, akielezea kusikitishwa kwake na kubaguliwa kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu. Cheptumo anasisitiza kuwa watoto walemavu wanahaki sawa na wenzao na kuwataka wazazi kuhakikisha wanapata elimu na huduma za matibabu bila ubaguzi. Cheptumo alisema haya kwenye uzinduzi wa awamu ya pili ya matembezi ya kilomita tano yanayotarajiwa kufanyika tarehe 14 Februari, katika shule ya watoto ywasioskia na kuona,Kabarnet. Cheptumo amewataka watu kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha watoto hawa wanapata raslimali zitakazowasaidia kuimarisha maisha yao.