Skip to main content
Skip to main content

Jenerali Kiambati wa Njora afariki akiwa na miaka 106 Nyandarua

  • | Citizen TV
    250 views
    Duration: 1:46
    Wakaazi wa Kaunti ya Nyandarua wanaomboleza kifo cha shujaa Kiambati wa Njora, Jenerali wa mwisho wa Mau Mau, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 106 nyumbani kwake Ngorika, Ol Kalou, Kaunti ya Nyandarua. Familia yake imethibitisha kuwa alifariki kwa amani kutokana na uzee, na mwili wake umehamishwa hadi makafani ya Umash mjini Nakuru. Kiambati wa Njora alikuwa miongoni mwa majenerali 12 wa Mau Mau wa kaunti ya Nyandarua waliopanga na kuongoza mapambano dhidi ya ukoloni wa Uingereza katika miaka ya 1950.