Jeshi la Ulinzi la Kenya limeanzisha mfumo mpya wa kidijitali wa uajiri katika shughuli inayoendelea ya kuwasajili makurutu wa jeshi kote nchini. Akiongea wakati wa shughuli hiyo katika uwanja wa Ihura, eneo la Murang’a Mashariki,Luteni Kanali Gabriel Kotikot alisema kuwa mfumo huo mpya unawawezesha maafisa kunasa taarifa za waliotuma maombi ya ajira kwa njia ya kielektroniki na kung’amua njama za udanganyifu mara moja. Kotikot alieleza kuwa watakaofaulu mchujo wa usajili watapokea barua za mwaliko kupitia barua pepe na jumbe fupi wala sio barua zilizotumika hapo awali. Kotikot alisisitiza kuwa mchakato huo utabaki kuwa wa haki na uadilifu ili kuhakikisha kuwa ni wale wanaofaa pekee ndio watasajiliwa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive