- 30,276 viewsDuration: 3:09Kinara wa ODM Dkt. Oburu Oginga sasa amebadili msimamo na kusema kuwa chama cha chungwa kitaelekea kwenye mazungumzo na chama cha UDA kikitafuta kupewa nafasi ya naibu rais. Hii ni kinyume na hapo awali ambapo alimhakikishia Naibu Rais profesa Kithure Kindiki kuwa odm haimezei mate kiti chake. Akizungumza kwenye mkutano na wajumbe wa odm kaunti ya Mombasa, Oginga amesema kuwa alinukuliwa visivyo, akisisitiza kuwa chama hicho kinatafuta kujiimarisha kikijiandaa kwa uchaguzi wa mwaka ujao