Jinsi ardhi ya kutetemeka huvutia watalii wengi kaunti ya Nakuru

  • | Citizen TV
    1,735 views

    Eneo moja katika wadi ya Kihingo ya Njoro,kaunti ya Nakuru limekuwa kivutio cha watalii na hata wakaazi kutokana na asili ya kipekee ya ardhi hiyo ambayo hutetema mtu anapotembea au hata kuruka juu yake. Kwa wakaazi wa eneo hili, Ardhi hii waliyoibandika jina ‘Kainaini’ inaweza kuhifadhiwa na kuwa kivutio kwa watalii wengi.