JSC yakashifu kukamatwa kimabavu kwa kiongozi wa DCP Peter Kawanjiru

  • | Citizen TV
    1,023 views

    Idara ya mahakama imekashifu kitendo cha maafisa wa kupambana na ugaidi kumkamata kimabavu kiongozi wa vijana w achama cha DCP Peter Kinyanjui Kawanjiru alipokuwa aliondoka katika mahakama ya Ruiru. Kwenye taarifa yake, tume ya huduma za mahakama - JSC - imewashtumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi na haswa kufyatua risasi kwenye majengo ya mahakama ya ruiru siku ya ijumaa wakati walipokuwa wakimkamata Kawanjiru baada ya mahakama kumwachilia kwa dhamana.