- 35 viewsDuration: 2:19Katika juhudi za kuwawezesha wanafunzi kuwa mstari wa mbele katika kuandika na kuhifadhi deta muhimu za utamaduni wa taifa la Kenya mitandaoni, shirika la Wikimedia Usergroup Kenya limezindua klabu ya kwanza katika taasisi ya elimu nchini katika chuo kikuu cha Pwani mjini Kilifi. Akizungumza na wanahabari katika hafla hiyo mkurugenzi mtendaji wa shirika la Wikimedia Kenya Winnie Kabintie amesema mchakato huo utasaidia kueleza kuhusu utamaduni kwa njia mwafaka na uhalisia.