Machifu na manaibu wao kwenye gatuzi la Nairobi walitofautiana na wasimamizi wa vituo vya polisi nchini almaarufu OCS, kuhusiana na juhudi za kukabiliana na biashara na uraibu wa mihadarati pamoja na pombe haramu huku machifu wakidai wasimamizi hao wanahujumu juhudi hizo. Kwa kujibu madai hayo wakati wa kikao cha Jukwaa La Usalama, waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen alisema maafisa wa utawala wa serikali ya kitaifa na polisi wanapaswa kushirikiana katika azma ya kutokomeza uhalifu na kufanikisha utoaji huduma kwa wananchi. Makala hayo ya Nairobi ni kilele cha vikao vya mazungumzo ya kushirikisha umma katika masuala ya usalama yaliyoandaliwa kote nchini ambayo yalifanyika katika magatuzi-46 kwa zaidi ya muda wa miezi sita iliyopita. Giverson Maina anaarifu zaidi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive