Skip to main content
Skip to main content

Jumba la Wamatangi karibu na uwanja wa Nyayo labomolewa

  • | KBC Video
    7,776 views
    Duration: 1:06
    Wamiliki wa biashara kwenye jumba la Prime Cleanshine karibu na uwanja wa Nyayo wanakadiria hasara kubwa baada ya matingatinga yakisimamiwa na zaidi ya maafisa elfu-2 wa polisi kubomoa jumba hilo leo asubuhi. Yadaiwa kwamba mali hiyo inahusishwa na gavana wa kaunti ya Kiambu Kimani Wamatangi. Ubomoaji huo ulianza mwendo wa saa tisa usiku huku maduka na bidhaa za mamilioni ya pesa zikiharibiwa. Wafuasi wa gavana huyo wameshtumu shughuli hiyo wakiitaja kuwa iliyochochewa kisiasa huku wafanyabiashara walioathirika wakitoa wito kwa serikali kuingilia kati. Riziki za wengi ziliharibiwa huku wafanyabiashara ndogo ndogo wakiathirika zaidi Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive