Justin Muturi Adai Maisha Yake Yamo Hatarini Baada ya Walinzi Kuondolewa

  • | K24 Video
    1,323 views

    Aliyekuwa Waziri wa Huduma za Umma na Mwanasheria Mkuu, Justin Muturi, anadai kuwa maisha yake yako hatarini baada ya serikali kuondoa walinzi wake. Haya yanajiri siku chache tu baada ya Muturi kumshutumu Rais William Ruto kwa kuongoza serikali inayokumbatia ufisadi. Akizungumza na waandishi wa habari, Muturi amesema hatakubali kutishwa na atabaki kuwa imara katika kusimamia ukweli.