Skip to main content
Skip to main content

Kalonzo ataka ukaguzi wa usalama katika shule za bweni

  • | Citizen TV
    307 views
    Kinara wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, ameitaka serikali kufanya ukaguzi wa dharura wa usalama katika shule zote za bweni nchini ili kuhakikisha zinazingatia viwango vya usalama na kuzuia vifo pamoja na majeraha yanayotokana na majanga ya moto. Kalonzo amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha usalama wa wanafunzi na kuzuia matukio yanayoweza kuepukika katika taasisi za elimu. Aidha, amependekeza kuanzishwa kwa mpango wa kitaifa wa ushauri nasaha unaofadhiliwa na serikali ili kuwasaidia wanafunzi kukabiliana na changamoto za maisha na kupunguza visa vinavyoongezeka vya migomo na machafuko shuleni. Kauli yake inajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama wa wanafunzi katika shule za bweni nchini.