- 7,428 viewsDuration: 2:36Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amewashtumu polisi akisema kuwa wanashirikiana na wahuni kuvuruga mikutano ya wanaoikosoa serikali. Kalonzo amewataka polisi kuwalinda wananchi badala ya kuwa chanzo cha fujo. Haya ni huku aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua akimshutumu rais William Ruto kwa kile anachosema ni kupuuza jamii ya wakalenjin katika maendeleo. Gachagua ambaye alikuwa akizungumza na wanahabari kutoka jamii hiyo amesema katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono kwenye uchaguzi mkuu ujao, rais amezipa jamii zingine umuhimu zaidi katika maendeleo