Kamati ya seneti yamhoji Afisa Mkuu wa EABL Jane Karuku

  • | Citizen TV
    631 views

    Mkurugenzi mkuu wa East African Breweries Limited Jane Karuku ameitetea kampuni hiyo dhidi ya madai ya ulaghai wa shughuli za umiliki wa hisa zake. AKIZUNGUMZA mbele ya Kamati ya Seneti ya Biashara, Viwanda na Utalii inayochunguza madai hayo, Karuku ametetea uamuzi wa hivi majuzi wa kuiuzia kampuni ya Diageo PLC asilimia 15% za hisa za East African Breweries Limited, akiutaja kuwa uwekezaji mzuri wa kibiashara. Kamati hiyo ilitaka kujua sababu za kampuni hiyo kuendelea kuuza mali yake na kuwapiga kalamu wafanyakazi wengi.