- 3,080 viewsDuration: 1:30Kamishina wa kaunti ya Garissa Ramadhan Mwabudzo amepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hii leo mjini humo ya kushinikiza kukamatwa kwa afisa wa DCI aliyempiga risasi na kumuuwa dereva wa taxi siku ya jumanne. Akizungumza ofisini mwake baada ya mkutano na wakuu wa usalama pamoja na viongozi wa kaunti hiyo, Mwabudzo amesema tayari uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo na hivyo maandamano yatachangangia hasara zaidi.