Skip to main content
Skip to main content

KAMPENI YA UTUPAJI SALAMA WA NEPI

  • | KNA Video
    40 views
    Duration: 2:34
    Mashirika Yahimizwa Kuunga Mkono Kampeni Ya Utupaji Salama Wa Nepi Za Watoto Mashirika mbali mbali yamehimizwa kuunga mkono kampeni ya kukumbatia utupaji salama wa nepi za watoto zilizotumika inayoendelezwa katika baadhi ya maeneo bunge kaunti ya Kilifi. Wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo katika eneo la Vipingo eneo bunge la Kilifi Kusini maafisa wa afya pamoja na manuspaa ya Mtwapa wamesema kuwa licha ya kampeni hiyo inayoendelea kutoa hamasa kwa wakazi kuhusu athari za utupaji kiholela wa nepi za watoto zilizotumika, imebainika kuwa mashirika na wadau wengine hawajajitokeza kuunga mkono kampeni hiyo.