- 2,100 viewsDuration: 35sMwasisi mwenza wa kampuni ya AI ya Anthropic, Jack Clark, ameonya kuhusu "hatari kubwa" zinazotokana na Akili unde (AI) na kutoa wito kwa serikali kuingilia kati. Akizungumza na BBC, ameonya kwamba teknolojia hiyo hivi karibuni inaweza kuleta hatari zisizotabirika. Anthropic ni moja ya kampuni zilizo mstari wa mbele katika mapinduzi ya akili unde na ndiyo iliyotengeneza chatbot ya Claude. Hatua hii inafuatia maonyo sawa na hayo kutoka kwa watu wengine wa ndani wa sekta hiyo, pamoja na maoni ya Rais Donald Trump yaliyopunguza uzito wa hatari hizo. #bbcswahili #AI #claude #anthropic Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw