Kampuni za maji za Nairobi na Athi zalaumiwa kwa uchafuzi wa Mto Nairobi

  • | Citizen TV
    414 views

    Waziri wa Mazingira Aden Duale ameonya kampuni zinazotengeneza bidhaa dhidi ya uchafuzi wa mto Nairobi akisema kuwa hatua zote za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Katika mkutano na washikadau, Duale ameitaka mamlaka ya mazingira - nema- kuwajibika na kuhakikisha kuwa sheria za mazingira zinafuatwa kikamilifu.kulingana na duale, mpango wa kusafisha mto nairobi utatimia tu iwapo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wanaouchafua.aidha duale amewatahadharisha wale wanaobeba takataka dhidi ya kusafirisha uchafu huo kwa kutumia magari yasiyofunikwa.