- 5,208 viewsDuration: 3:04Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kanini Kega leo ameandikisha taarifa katika Kituo cha Polisi cha Ol-Joro-Orok, Kaunti ya Nyandarua, kufuatia madai ya kuvamiwa kwa gari lake katika eneo hilo jana usiku. Kega alidai tukio hilo lilitokea alipokuwa akitoka katika mkutano wa kisiasa wa chama cha DCP katika eneo bunge la Ol Kalou. Hata hivyo, dereva wa Kega alikamatwa kwa kuendesha gari hilo ambalo halikuwa na nambari ya usajili.