Skip to main content
Skip to main content

Kasisi Michael Mutiso azuru kaunti 37 kuhamasisha umma dhidi ya mihadarati

  • | Citizen TV
    608 views
    Duration: 2:04
    Katika juhudi ya kukomesha matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana humu nchini kasisi mmoja kwa jina la utani Bishop wa Bike amezuru kaunti 37 akitumia pikipiki maalum kuhamasisha umma dhidi ya matumizi ya dawa hizo. Kasisi Michael Mutiso wa kanisa la Gospel Outreach Children anasema alianza harakati ya kutoa hamasisho kote nchini kufuatia kifo cha mwanawe kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Akizungumza na wanahabari baada ya kuzuru kaunti ya Kilifi Kasisi Mutiso amesema aliamua kutumia pikipiki ili aweze kupenya maeneo mbali mbali na pia kutangamana kwa urahisi na vijana ambao wengi wao ni wanabodaboda.