Katibu Mkuu wa chama cha ODM Sifuna asema maandamano yatafanyika kwa siku tatu mfululizo wiki ijayo

  • | Citizen TV
    2,873 views

    Katibu Mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna amesema kuwa maandamano wiki ijayo yatafanyika kwa siku tatu mfululizo. Akizungumza na runinga ya Citizen kwenye kipindi cha daybreak, Sifuna amesema kuwa Azimio haitakoma kushinikiza mabadiliko ya kushuka kwa gharama ya maisha na kuwa maandamano yatafanyika kuanzia Jumatatu hadi Jumatano wiki ijayo.