Kaunti ya Busia kulima zaidi ya ekari 20,000 za mashamba

  • | Citizen TV
    282 views

    Serikali ya kaunti ya Busia inalenga kulima zaidi ya ekari 20,000 za mashamba kufikia mwishoni mwa msimu huu wa upanzi, ili kuimarisha uzalishaji wa chakula. Gavana wa kaunti hiyo Paul Otuoma amezindua tinga tinga za kaunti hiyo zitakazowalimia mashamba wakazi kwa gharama nafuu. Otuoma amesisitiza nia yake ya kuhakikisha kuna chakula cha kutosha katika kaunti hiyo.