Skip to main content
Skip to main content

Kaunti ya Embu yazindua mpango wa madaktari mashinani

  • | Citizen TV
    44 views
    Duration: 2:41
    Serikali ya Kaunti ya Embu imezindua mpango wa kuwafikishia wakazi wa maeneo ya mashinani huduma za maalum za afya. Kupitia mpango huo unaojulikana kama “Madaktari Mashinani,” Idara ya Afya itakuwa ikipeleka madaktari kutoa huduma mbalimbali ikiwemo ushauri wa kitaalamu, uchunguzi wa kina pamoja na huduma nyinginezo za afya. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika Kituo cha Afya cha Gategi, eneo bunge la Mbeere kusini, Afisa Mkuu wa Afya ya Umma Henry Nthiga alisema kuwa mpango huo unalenga kusongeza huduma maalum za afya karibu na wananchi badala ya kutegemea hospitali kubwa kama ile ya rufaa ya Embu. Alibainisha kuwa wagonjwa wengi wa maeneo ya mashinani wamekuwa wakikosa kufika hospitali hizo kutokana na gharama kubwa na umbali mrefu. Wagonjwa waliopokea huduma hizo wameeleza kufurahishwa na mpango huo, wakisema umewapunguzia gharama na usumbufu wa kusafiri mbali kutafuta huduma za kibingwa.