Kaunti ya Kajiado ni moja ya kaunti ambazo hukumbwa na kiangazi

  • | K24 Video
    38 views

    Kaunti ya Kajiado ni moja ya kaunti ambazo hukumbwa na kiangazi mara kwa mara kila kunapokuwa na mvua kidogo au inapokosekana kabisa. Huku ikizingatiwa kuwa jamii ya maasai hutegemea sana mifugo kama kitega uchumi, wengi hufa kila kiangazi kinapokuwa cha muda mrefu. Hata hivyo kufuatia utafiti na mafunzo ya jinsi ya kupunguza hasara ya mifugo wao wakati wa kiangazi, wengi wamefaidika.