- 43 viewsDuration: 1:12Kaunti ya Kilifi ndiyo itakuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Ukame, baada ya Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) kubaini kuwa eneo hilo ni miongoni mwa kaunti zinazokumbwa zaidi na changamoto za kimazingira nchini. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa NEMA, Dkt. Charles Lange, hafla hiyo itawaleta pamoja washikadau wa kitaifa na kimataifa, na kutoa jukwaa muhimu la kubuni mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto sugu za kimazingira, hususan ukame.