Kenya imepokea msaada wa vifaa vya matibabu vya thamani ya shilingi milioni 65

  • | Citizen TV
    554 views

    Kenya imepokea msaada wa vifaa vya matibabu vya thamani ya shilingi milioni 65 kupiga jeki sekta ya afya nchini. Msaada huu kutoka kwa serikali ya Ujerumani inajumuisha kliniki tatu tamba, kliniki nyingine nne na hata majokofu ya safari. Msaada huu zaidi utasaidia utoaji wa chanjo haswa maeneo ya kaskazini mwa Kenya. Waziri wa afya Susan Nakhumicha amesema msaada huu utachangia mpango wa afya kwa wote huku mkewe Rais Rachel Ruto akisema vifaa hivi vitasaidia kuhakikisha watoto wote nchini wanapata chanjo