2,208 views
Duration: 3:26
Kenya imeafikia makubaliano na Senegal yanayolenga kuondoa hitaji la visa kwa wasafiri kati ya nchi hizo mbili. Mkataba huo ulitiwa saini katika Ikulu ya Nairobi wakati wa ziara ya kitaifa ya Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye humu nchini. Kupitia makubaliano hayo, raia wa Kenya na wale wa Senegal watakuwa huru kusafiri kati ya nchi hizo bila visa kwa muda wa siku 90. Aidha, Maraisi hao walijadili sekta nyingine za ushirikiano ikiwa ni pamoja na biashara, kawi na juhudi za kuleta amani. Nancy Okware anatuarifu kwa kina kuhusu yaliyojiri katika ikulu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive