- 255 viewsDuration: 56sKesi ya mauaji ya mwalimu na mwanablogu Albert Omondi Ojwang imeendelea leo katika Mahakama Kuu ya Kibera huku shahidi aliyelindwa wa upande wa mashtaka akiendelea kuiongoza mahakama kupitia picha za kamera za usalama, CCTV, zilizorekodiwa katika Kituo cha Polisi cha Nairobi Central usiku wa tarehe 7 kuamkia tarehe 8 Juni mwaka 2025.