Kijana wa miaka 18 apigwa risasi na kuuwawa na NPR

  • | Citizen TV
    1,564 views

    Wakazi wa eneo la Chepchoina kaunti ya Trans Nzoia wanalalamikia mauaji ya kijana mmoja ambaye anadaiwa kupigwa risasi na afisa wa polisi wa akiba -NPR- alipokuwa akichakura mabaki ya mahindi katika shamba la ADC Suam. Kijana huyo mwenye umri wa miaka kumi na minane anadaiwa kupigwa risasi mara mbili kifuani na afisa huyo. Na kama anavyoarifu Collins Shitiabayi, polisi wanasema wanachunguza kisa hicho kabla ya kuchukua hatua