- 6,845 viewsDuration: 3:38Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 27 kutoka bomet amekamilisha safari ndefu ya kutembea zaidi ya kilomita 200 kutoka Bomet hadi Nairobi katika matumaini ya kuchangisha karo ya masomo yake ya chuo kikuu. Dancan Kibet, aliyemaliza elimu yake ya sekondari mwaka 2015, hajawahi kujiunga na chuo kikuu kwa zaidi ya mwongo mmoja kutokana na changamoto za kifedha. Sasa, miaka 11 baadaye, Kibet bado hajakata tamaa ya kutimiza ndoto yake.