- 4,421 viewsDuration: 2:38Ilikuwa furaha isiyo kifani katika kijijini Kirogo eneo la Mwea kaunti ya Kirinyaga baada ya wakazi wa eneo hilo kujumuika kumkaribisha nyumbani mwanamke aliyeachiliwa baada ya kuhudumu miaka 27 gerezani. Beatrice Wanjiru, aliyefungwa akiwa na miaka 33 na ambaye sasa ana miaka 60, akisema ni furaha kubwa kuonana tena na wanawe baada ya kuachiliwa licha ya kufungwa maisha kwa mauaji.