Kina mama wachanga wafunzwa mbinu za kilimo katika kaunti ya Samburu

  • | Citizen TV
    365 views

    Hofu imeibuka kuhusu uchomaji wa makaa kaunti ya Samburu, ambapo kina mama wengi wamegeukia kazi hii kukidhi mahitaji ya familia zao. Kutokana na hali hii wanaharakati na wanamazingira wameanza mafunzo kwa kina mama hawa kugeukia kilimo ili kujiepusha na uchomaji makaa unaosababisha athari kwa mazingira na afya.