Skip to main content
Skip to main content

Kinamasi Cha Kware: Matukio ya mauaji ya Kware Pipeline

  • | Citizen TV
    10,441 views
    Duration: 9:58
    Imekuwa zaidi ya mwaka mmoja tangu kutambuliwa kwa miili ya wanawake waliouawa kwa mtindo sawa katika timbo za Kware eneo la Pipeline mwaka jana, safari ya haki imekwama kwa jamaa za waathiriwa. Mshukiwa wa mauaji Collins Jumaisi akisalia kuripotiwa kutoweka seli tangu mwaka jana, maswali ya haki yameendelea kutoka kwa jamaa na hata wanaharakati. Mwanahabari wetu Franklin Wallah anaangazia tukio hili zaidi ya mwaka baadaye, akiangazia jinsi familia zilivyowachwa solemba kutafuta haki, kwenye makala yetu maalum ya 'Kinamasi cha Kware'