Kinara wa DCP adai Raila anawapotosha wafuasi wake

  • | Citizen TV
    2,057 views

    Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua amemsuta kinara wa ODM Raila Odinga kwa kile anasema ni kuwapotosha wafuasi wake na kuwatumia kama kivukio cha kuingia serikalini. Akizungumza katika mkutano wa wakenya wanaoishi mjini Anaheim Carlifonia kusini nchini Marekani, Gachagua amesema muda umewadia wa wakenya kuwafurusha Odinga na Rais William Ruto kwenye ulingo wa siasa katika uchaguzi mkuu wa 2027.