- 1,063 viewsDuration: 1:49Kinara wa chama cha United Green Movement, David Maraga, ameikosoa serikali kuhusu matumizi ya vitoa machozi katika mikutano ya kisiasa ya upinzani. Akizungumza akiwa katika ziara ya kaunti ya Meru, Maraga amesema anaunga mkono wito wa upinzani unaomtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, kuwachukulia hatua maafisa wanaodaiwa kuhusika na matukio hayo. Aidha, Maraga ameeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa ukame na njaa nchini, akidai serikali haijapata suluhisho mwafaka la kukinga wananchi dhidi ya madhara hayo huku maeneo mengi yakiendelea kukumbwa na hali hiyo.