Kindiki: Mrundiko wa pasipoti umepungua hadi 40,000

  • | Citizen TV
    1,034 views

    Waziri wa usalama Profesa Kithure Kindiki sasa anasema kuwa mrundiko wa vyeti vya uhamiaji utaisha katika muda wa siku kumi zijazo. Kindiki ambaye alifanya ziara ya ghafla kwa mara ya tatu katika idara ya uhamiaji katika jumba la nyayo hapa jijini Nairobi, anasema mrundiko wa pasipoti umepungua hadi elfu 40,000. Prof Kindiki ameongeza kuwa mikakati ambayo imeratibiwa kuimarisha uchapishaji wa pasipoti utapunguza muda wa kupiga foleni hadi dakika 30 kutoka zaidi ya saa mbili. Kadhalika kindiki amesikitishwa na hali ya kujikokota wakati wa kutafuta cheti cha maadili katika idara ya upelelezi na kuahidi kushughulikia suala hilo .