Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kukutana na Rais Putin katika ziara yake Russia

  • | VOA Swahili
    1,170 views
    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametumia treni yenye rangi ya kijani iliyokoza kusafiri kwenda Russia, vyombo vya habari vya serikali vimeionyesha safari hiyo Jumanne (Septemba 12). Kim akitegemea usafiri wa pole pole lakini aina maalum ya usafiri ambao viongozi waliojitenga wa nchi hiyo wamekuwa wakiutumia kwa miongo kadhaa. Ikilinganishwa na ndege kongwe za nchi hiyo, treni yenye kizuizi cha risasi kupenya inatoa usafiri salama zaidi na usiochosha kwa msafara mkubwa, walinzi, chakula na mahitaji mengine, na mahali pa kujadili ajenda kabla ya mikutano. Afisa wa zamani wa Korea Kaskazini ambaye alikuwemo katika treni hiyo ya Muasisi wa Korea Kim II Sung, Ko Young Hwan, aliiambia Reuters Jumanne. Tangu alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2011, Kim ametumia treni kuzuru China na Vietnam, na pia ziara zake za zamani alizofanya huko Russia alipokutana na Putin mwaka 2019. - Reuters/KRT #kimjongun #koreakaskazini #treni #russia #rais #putin #voa #voaswahili #dunianileo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.