Kiwanda cha sukari cha Sony Sugar kimepanga kuanza tena shughuli zake za kusaga miwa baada ya kukamilisha mpango wa kukarabati vifaa vyake. Shughuli hiyo iliyogharimu shilingi milioni 800 inalenga kutatua matatizo ya miaka mingi, na kuimarisha uzalishaji ..
Wasimamizi wa kampuni hiyo wanasema mashine za zamani ambazo hazikutengenezwa kabla ya ubinafsishaji ziliendelea kuleta uharibifu na kuvuruga uzalishaji thabiti, na kusababisha wasiwasi kuhusu uendelevu wa kiwanda....
Aidha Usimamizi upya wa Kampuni hiyo pia umeeleza kuwa wamenunua pikipiki mpya kwa ajili ya maafisa wa mashinani wanaotembelea wakulima walio na mikataba…...