KNUT yaitaka KNEC kuwalipa wasahihishaji wa mitihani

  • | Citizen TV
    345 views

    Chama cha walimu KNUT kimeonya bodi ya kusimamia mtihani KNEC dhidi ya kuchelewesha kwa marupurupu ya walimu wanaosimamia mtihani wa kidato cha nne na darasa la nane. Akizungumza katika eneo la karachuonyo katibu wa kitaifa wa KNUT Collins Oyu amesisitiza kwamba haki ya walimu lazima iheshimiwe. Haya yanajiri wakati ambapo walimu wengi hasa mashinani wakiitaka serikali kuwapandisha cheo waliohitimu.