Kongamano la kuangazia nafasi ya teknolojia kwa maji lafanyika Mombasa

  • | Citizen TV
    116 views

    Kongamano la maji linaloendekea katika kaunti ya Mombasa limeingia siku ya pili hii leo. Kongamano hilo lililozinduliwa rasmi na Naibu rais Rigathi Gachagua linalenga kutumia teknolojia na ubunifu wa kisasa kutosheleza uhaba wa maji unaoendelea kuchangiwa na mabadiliko ya tabia nchi. Waziri wa Maji Alice Wahome ametaka serikali kuu serikali za kaunti na hata wawekezaji katika sekta ya maji kupunguza uharibifu na kushirikiana kuimarisha sekta hii.