Konokono adimu atoa yai

  • | BBC Swahili
    867 views
    Kwa mara ya kwanza, konokono huyu akitoa yai kutoka chini ya kichwa chake amerekodiwa, kwa mujibu wa shirika la uhifadhi la New Zealand. Konokono hawa hupatikana tu New Zealand, hasa katika misitu na maeneo ya miinuko yenye nyasi, ambapo wanakabiliwa na hatari ya kupoteza makazi yao. Sehemu kubwa ya makazi yao imeharibiwa na uchimbaji madini. Wengi wao, kama huyu, huwekwa kwenye hifadhi baridi yenye mazingira yanayofanana na asilia yao ili kusaidia kuhifadhi spishi hiyo, ambayo huzaliana polepole na haizoei mazingira mapya kwa urahisi. #bbcswahili #newzealand #mzingia Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw