KORIR ASEMA MASLAHI YA WANARIADHA YAPEWA KIPAUMBELE

  • | K24 Video
    29 views

    Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Nairobi, Barnaba Korir, amesema maslahi ya wanariadha na wachezaji yanapaswa kupewa kipaumbele na Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki (NOCK). Korir alizungumza pamoja na Naibu Rais wa Kwanza wa NOCK, Shadrack Maluki, ambaye anakutana na ushindani mkali kutoka kwa Katibu Mkuu, Francis Mutuku, katika kinyang’anyiro cha nafasi ya juu ya uongozi. Matokeo ya uchaguzi wa viongozi hao yataamuliwa na wajumbe 29 kutoka mashirikisho yaliyosajiliwa.