Skip to main content
Skip to main content

Koskei awahimiza wazazi kushiriki elimu ya watoto

  • | KBC Video
    64 views
    Duration: 1:33
    Mkuu wa utumishi wa umma, Felix Koskei, amewataka wazazi kuendelea kushiriki kikamilifu katika elimu ya watoto wao kwa kuwapa mwongozo, motisha na msaada unaohitajika ili waweze kufanikiwa. Akizungumza alipofungua rasmi jumba jipya la kisasa la maakuli lililojengwa kwa ufadhili wa wahisani katika shule ya sekondari ya wasichana ya Friends Moi Kaptama, katika eneo la Mlima Elgon, Koskei amesema elimu ndio njia ya uhakika ya kupanua fursa, kuimarisha maendeleo ya kijamii na kukomesha matukio ya vurugu. Aidha, ametoa wito kwa jamii kushirikiana kukabiliana na tatizo la ulevi, akisema bado ni changamoto kubwa inayolikabili eneo hilo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive