KRA yasema haiwezi kufutilia mbali madeni ya kampuni za sukari

  • | Citizen TV
    393 views

    Mamlaka ya ushuru -KRA- imesema kuwa haina uwezo wa kisheria kufutilia mbali deni la shilingi bilioni 36.7 ambazo kampuni za sukari humu nchini zinadaiwa. Kwenye kikao cha pamoja cha kamati za bunge kuhusu fedha na kilimo, kamishna wa ushuru Rispah Simiyu alisema kuwa sheria ya fedha ya mwaka 2023 ilifutilia mbali uwezo wa KRA kuchukua hatua kama hizo. simiyu hata hivyo amesema kuwa KRA ina uwezo wa kufutilia mbali faini na riba zinazotokana na kutolipwa kwa madeniyaliyokuwepo kabla ya iwsho wa disemba 2022.kampuni ya Mumias sugar inadaiwa shilingi bilioni 20.2 B za malimbikizi ya ushuru, Nzoia shilingi bilioni 7.2, Muhoroni shilingi bilioni 3.2, Sony shilingi bilioni 3.2, Chemelil shilingi bilioni 2.8 na Miwani shilingi bilioni 2.1.