Skip to main content
Skip to main content

‘Kumwaga damu ya mtu mmoja asiye na hatia si baraka’

  • | BBC Swahili
    24,509 views
    Duration: 1:51
    ‘Kumwaga damu ya mtu asiye na hatia si baraka katika taifa’ - Mwigulu Nchemba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchembe amewasihi Watanzania kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiunga mkono Tume aliyoiunda kuchunguza vurugu za Oktoba 29, 2025. Amesema tukio hilo limeleta msukosuko nchini, likihusisha vifo na madhara kwa baadhi ya watu, jambo ambalo linapaswa kuwa funzo kwa taifa. Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Novemba 25, 2025, wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. “Baada ya kumaliza uchaguzi, kulitokea vurugu ambazo zimegharimu maisha ya baadhi ya watu. Katika imani yangu, kumwaga damu ya mtu asiye na hatia ni jambo zito. Ombi langu ni kwamba kila mmoja katika dhamira yake anatamani tusirudie kamwe jambo kama hili. Linatuachia makovu yasiyopona,” amesema. Dk Mwigulu amesema ni muhimu Watanzania wote kuungana na Rais Samia ili kupata uhalisia wa kilichotokea kupitia tume hiyo, ambayo imeundwa na watu wenye weledi na heshima katika jamii. Amesisitiza kuwa kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni, lakini ni vyema kutambua kuwa wajumbe wa tume hiyo ni watu wa kuaminika na wenye uzoefu mkubwa katika masuala ya kisheria, hivyo wanastahili kupewa nafasi ya kufanya kazi yao bila kuingiliwa. - - #bbcswahili #tanzania #siasa #maandamano #uchaguzimkuu2025