- 588 viewsDuration: 3:00Chama cha walimu wa shule za sekondari KUPPET kimeelekezea kidole cha lawama Wizara ya Elimu kwa mkasa wa moto katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Utumishi. KUPPET inadai kuwa Wizara ya Elimu iliruhusu wanafunzi wengi kupita kiasi kujiunga na Gredi ya Kumi licha ya shule hiyo kukosa nafasi. Aidha, KUPPET pia inasema kuwa wizara imekuwa ikiruhusu kuhamishwa kwa wanafunzi kutoka shule zingine hadi shule hiyo licha ya malalamiko kutoka kwa mwalimu mkuu.