- 591 viewsDuration: 4:00Je, wajua kwamba kila mwaka binadamu huchangia taka tani bilioni 2.3? Kulingana na shirika la mazingira katika umoja wa mataifa unep, iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa huenda taka hizi zikaongezeka kufikia tani bilioni 3.8 ifikapo mwaka wa 2050. Hata hivyo, kuna mashirika humu nchini kama vile hospitali ya rufaa ya chuo kikuu cha kenyatta ambayo imeweka mikakati maalum kuzuia madhara yanayotokana na utupaji taka kuambatana na mwongozo wa wizara ya afya.