Kwa nini watu wengi wamefariki kutokana na mafuriko Afrika Mashariki?

  • | BBC Swahili
    1,132 views
    Watu 114 wamefariki katika jimbo la Kivu Kusini huko DRC, ambapo mto Kasaba unaopeleka maji yake katika ziwa Tanganyika umevunja kingo zake na kusababisha mafuriko. Nchini Somalia, mamlaka zimesema kwamba mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa usiku wa Ijumaa yamesababisha vifo vya watu 7 jijini Mogadishu. Nchini Kenya, shirika la msalaba mwekundu limeripoti kwamba makazi elfu 10 yameathiriwa na mvua kubwa inayonyesha hasa katika maeneo ya pwani na kwengineko nchini humo. Na nchini Tanzania, athari ya mvua kubwa imeshuhudiwa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo watu 3 wamepoteza maisha huku nyumba na barabara zikiharibiwa vibaya.