- 211 viewsDuration: 1:40Serikali kupitia wizara ya madini imetangaza mchakato wa kupatikana kwa haraka kwa leseni za uchimbaji madini kaunti ya Taita Taveta baada ya wachimbaji madini kusubiri kwa muda mrefu. Katibu katika wizara hiyo Harry Kimtai akizungumza huko Kishushe wakati wa kutiwa saini mkataba wa uchimbaji madini kati ya kampuni ya Devki na shamba la kijamii la Kishushe anasema serikali iko tayari kuhakikisha sekta ya uchimbaji madini inaboreshwa.